Galatians 1

Salamu

1 aPaulo mtume: si mtume wa wanadamu wala aliyetumwa na mwanadamu, bali na Isa Al-Masihi na Mungu Baba aliyemfufua Isa kutoka kwa wafu; 2 bna ndugu wote walio pamoja nami:

Kwa makanisa ya Galatia:

3 cNeema iwe nanyi na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi, 4 daliyejitoa kwa ajili ya dhambi zetu ili apate kutuokoa katika ulimwengu huu wa sasa ulio mbaya, sawasawa na mapenzi yake yeye aliye Mungu na Baba yetu. 5 eUtukufu una yeye milele na milele. Amen.

Hakuna Injili Nyingine

6 fNashangaa kwamba mnamwacha upesi hivyo yeye aliyewaita kwa neema ya Al-Masihi na kuifuata Injili nyingine, 7 gambayo kwa kweli si Injili kamwe, ila kwa dhahiri kuna watu wanaowachanganya na wanaotaka kuipotosha Injili ya Al-Masihi. 8 hLakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri Injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo alaaniwe milele! 9 iKama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu yeyote atawahubiria Injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!

10 jJe, sasa mimi ninatafuta kukubaliwa na wanadamu au kukubaliwa na Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa bado najaribu kuwapendeza wanadamu, nisingekuwa mtumishi wa Al-Masihi.

Paulo Ameitwa Na Mungu

11 kNdugu zangu, nataka mjue kwamba Injili niliyowahubiria haikutokana na wanadamu. 12 lKwa maana mimi sikuipokea hiyo Injili kutoka kwa mwanadamu, wala sikufundishwa na mtu, bali niliipata kwa ufunuo kutoka kwa Isa Al-Masihi.

13 mNinyi mmekwisha kusikia juu ya maisha yangu ya zamani nilipokuwa katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu kwa nguvu na kujaribu kuliangamiza. 14 nNami niliendelea sana katika dini ya Kiyahudi kuliko Wayahudi wengi wa rika yangu maana nilijitahidi sana katika desturi za baba zangu. 15 oLakini ilipompendeza Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu na kuniita kwa neema yake, 16 palimdhihirisha Mwanawe kwangu, ili nipate kumhubiri miongoni mwa watu wa Mataifa. Mimi sikushauriana na mwanadamu yeyote, 17 qwala sikupanda kwenda Yerusalemu kuwaona hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nilikwenda mara moja Arabuni na kisha nikarudi Dameski.

18 rKisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kuonana na Kefa
Yaani Petro.
na nilikaa naye siku kumi na tano.
19 tLakini sikumwona mtume mwingine yeyote isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. 20 uNawahakikishia mbele za Mungu kuwa ninayowaandikia si uongo. 21 vBaadaye nilikwenda sehemu za Syria
Syria hapa ina maana ya Shamu.
na Kilikia.
22 xLakini mimi binafsi sikujulikana kwa makanisa ya huko Uyahudi yaliyo katika Al-Masihi. 23 yWao walisikia habari tu kwamba, “Mtu yule ambaye hapo kwanza alikuwa akitutesa sasa anahubiri imani ile ile aliyokuwa akijaribu kuiangamiza.” 24 zNao wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.
Copyright information for SwhKC